Unahitaji Kujua:

Tuma hadithi MOJA fupi ambayo haijachapishwa (chini ya maneno mia sita), na ungojee ujumbe kutoka kwetu kabla ya kutuma hadithi nyingine.

Andika waraka wenye wasifu wako ukitumia nafsi ya tatu, lakini usiweke jina lako kwenye hadithi yenyewe.

Hatupeani malipo, lakini tunajitolea kuwapa waandishi jukwaa.

Haki za uchapishaji kwenye mtandao: Tutahitaji haki za kipekee za kuchapisha kazi yako kwenye mtandao kwa miezi mitatu. Baada ya mda huo, tutahitaji haki zisizo za kipekee za kuweka kazi yako kwenye nyaraka za mtandao wetu.

Haki za uchapishaji kwenye vitabu: Tunahitaji haki zisizo za kipekee za kuchapisha kazi yako kwenye vitabu na katika matangazo yetu. Haki zingine zote zitabakia kuwa zako.

Sign up form

Please enter a valid email address.